1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi na Ukraine zashambuliana kwa droni na makombora

13 Oktoba 2024

Ukraine imesema siku ya Jumapili kuwa Urusi iliishambulia nchi hiyo kwa kuvurumisha jumla ya makombora manne na droni zipatazo 68.

Kifaru cha Urusi kikijianda kwa mashambulizi katika eneo la mpakani la Kursk
Kifaru cha Urusi kikijianda kwa mashambulizi katika eneo la mpakani la KurskPicha: Russian Defense Ministry/AP/picture alliance

Vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine vimeeleza kuwa vimeharibu karibu droni 31 huku 36 zikiaminika kuwa ziliharibikia angani. Makombora mawili ya masafa marefu ya Iskander-M yalipiga mikoa ya Poltava na Odesa huku mengine yakiilenga mikoa ya Chernihiv na Sumy.

Kwa upande wake wizara ya ulinzi ya Urusi imesema imeharibu droni 13 za Ukraine katika mikoa mitatu ya mpakani ambayo ni Belgorod Bryansk na  Kursk . Hayo yakiarifiwa, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema siku ya Jumamosi kuwa kwa msaada wa uwekezaji wa mataifa ya Magharibi, Kiev inalenga kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wake wa silaha ikiwa ni pamoja na droni na makombora.