Urusi na Ukraine zashambuliana, watu wawili wauwawa
20 Machi 2026
Maafisa wametangaza kuwa mashambulizi ya usiku kucha kat ya Ukraine na Urusi yalitokea wakati rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipotangaza kwamba wapatanishi kutoka Kyiv walikuwa wakisafiri kwenda Marekani kwa lengo la kuanzisha tena mazungumzo ya pande tatu na Urusi.
Mkuu wa eneo la kusini mwa Ukraine la Zaporizhzhia alisema mashambulizi ya Urusi huko yalimuua mwanamke wa miaka 30 na kumjeruhi mvulana mmoja, 10, na mwanamume mmoja, 48.
Jeshi la anga la Ukraine lilitangaza kwamba Urusi ilikuwa imeshambulia nchi hiyo kwa kutumia ndege zisizo na rubani 156 na kwamba mifumo ya ulinzi wa anga ilikuwa imeziangusha 133 kati yao.
Shambulio la Urusi lililenga maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na mji wa bandari wa kusini wa Odesa ambapo maafisa walisema meli mbili za mizigo zilizojaa nafaka zilikuwa zimeharibiwa, na kwamba wafanyakazi wawili walijeruhiwa.