Urusi na Ukraine zashindwa tena kukubaliana usitishwaji vita
24 Julai 2025
Pande hizo mbili lakini bado zinatofautiana pakubwa linapokuja suala la usitishwaji mapigano na uwezekano wa kukutana kwa viongozi wao.
Mkuu wa ujumbe wa Ukraine Rustem Umerov baada ya mazungumzo hayo yaliyodumu kwa dakika 40 amesema, Ukraine imependekeza mkutano wa Rais Volodymyr Zelenskiy na Rais Vladimir Putin kabla mwishoni mwa mwezi Agosti.
Umerov amedai kuwa iwapo Urusi italikubali pendekezo hilo, basi itaonyesha mwelekeo wake wa kutaka usitishwaji vita.
Ila mkuu wa ujumbe wa Urusi Vladimir Medinskiy amesema, kukutana kwa viongozi wawili wa nchi hizo kunastahili kuwa hatua ya kutia saini makubaliano na wala isiwe kukutana kwa mazungumzo ya kila kitu kutoka mwanzo.
Medinskiy amesema Urusi inataka usitishwaji mapigano wa muda mfupi wa masaa 24 hadi 48 ila Ukraine inashikilia kwamba usitishwaji mapigano ufanyike mara moja na uwe wa muda mrefu.