Urusi ni mwenyeji wa mkutano wa BRICS mjini Kazan
22 Oktoba 2024Matangazo
Mkutano huo wa kilele wa siku tatu katika mji wa Kazan ndio mkubwa zaidi wa aina hiyo kufanyika nchini Urusi tangu ilipoanza mashambulizi yake nchini Ukraine. Wakuu wa nchi 24 na serikali wanahudhuria mkutano huo na miongoni mwo ni Rais wa China Xi Jinping, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Masuala makuu katika ajenda ya mkutano huo ni pamoja na wazo la Putin la mfumo wa malipo unaoongozwa na BRICS kwa ajili ya kushindana na mfumo wa SWIFT, ambao ni mtandao wa kimataifa wa kifedha uliosimamisha benki za Urusi kuendesha kazi zake mnamo mwaka 2022. Mzozo unaozidi kuongezeka katika Mashariki ya Kati pia ni miongoni mwa maswala yatakayozungumziwa.