1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Sera za Marekani zatishia matumizi ya nyuklia

8 Novemba 2023

Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi Nikolai Patrushev amesema hii leo kuwa sera za Marekani na washirika wake zinaongeza hatari ya kutumiwa kwa silaha za nyuklia, kemikali au kibayolojia.

Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi Nikolai Patrushev.
Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi Nikolai Patrushev.Picha: Iranian Presidency/ZUMA Press/picture alliance

Hayo yanajiri baada ya Marekani kutangaza hapo jana kuwa itajiondoa katika mkataba wa kudhibiti vikosivya kawaida barani Ulaya, CFE, baada ya Urusi nayo kujiondoa katika mkataba huo. 

Soma pia:Urusi yajiondoa kutoka kwenye uidhinishaji wa kupinga majaribio ya silaha za nyuklia

Wiki iliyopita, Urusi ilijiondoa pia katika mkataba wa kuzuia majaribio ya silaha za nyuklia, jambo linaloibua maswali kuhusu hatima ya mikataba ya udhibiti wa silaha barani Ulaya. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW