1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi: Kombora dhidi ya Ukraine onyo kwa nchi za Magharibi

Angela Mdungu
22 Novemba 2024

Ikulu ya Urusi, Kremlin imesema shambulio ililolifanya dhidi ya Ukraine kwa kutumia kombora jipya ni ujumbe kwa mataifa ya Magharibi kuwa Moscow itajibu maamuzi yao ya kukurupuka na namna yanavyoiunga mkono Ukraine.

DNIPRO, Ukraine
Eneo la Dnipro lililoshambuliwa na kombora la Urusi 22.11.2024Picha: Press Service of the State Emergency Service of Ukraine in Dnipr/picture alliance

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov ameyasema hayo Ijumaa siku moja baada ya Rais Putin kusema kuwa jeshi lake liliishambulia ngome ya kijeshi ndani ya Ukraine kwa kutumia kombora jipya la masafa marefu aina ya Oreshnik.

Akizungumza na wanahabari, Peskov amesema kuwa ujumbe mkuu wa shambulio hilo ni kuwa maamuzi ya kizembe na hatua za mataifa ya magharibi yanayozalisha makombora na kuyapeleka Ukraine na kutumiwa dhidi ya Urusi, haziwezi kukaliwa kimya.

Soma zaidi: Putin aonya kuwa vita vya Ukraine vinachukua mkondo wa kidunia

Amefafanua kuwa Urusi haina wajibu wa kuitahadharisha Marekani kuhusu shambulio hilo lakini iliamua kuitaarifu dakika 30 kabla ya kushambulia. Peskov amesema Rais Putin bado yuko tayari kwa mazungumzo ya usuluhishi ingawa alibainisha kwamba utawala wa Rais wa Marekani anayemaliza muda wake unapendela kuendelea na hatua ya kuuchochea mvutano huo.

Urusi ililishambulia eneo la Dnipro la Ukraine kwa aina mpya ya kombora Picha: Press Service of the State Emergency Service of Ukraine in Dnipr/picture alliance

Putin alisema Alhamisi kuwa Urusi ilirusha kombora lake jipya baada ya Ukraine kuishambulia Urusi kwa kutumia kombora la masafa marefu la Marekani aina ya ATAMCMS baada ya utawala wa Biden kuidhinisha hatua hiyo. Alidai pia kwamba makombora ya Uingereza aina ya Storm Shadow yalitumika kuishambulia nchi yake.

Kwa upande wake Rais wa Ukrainie Volodymyr Zelenskiy amesema kitendo cha Urusi kutumia kombora la kisasa kuishambulia nchi yake yanazidi kuchochea vita na kuwa kinapaswa kulaaniwa na dunia nzima.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW