1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Ukraine imekuwa ikitumia silaha za kemikali

18 Desemba 2024

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema leo kwamba Ukraine imekuwa ikitumia mara ya kwa mara kemikali ya sumu aina ya Phosphorous katika mashambulizi yake ya droni mnamo mwezi Septemba.

Russland Moskau | Maria Zakharova beim Forum für Multipolarität
Picha: Komsomolskaya Pravda/Russian Look/IMAGO

Msemaji wa wizara hiyo Maria Zakharova amesema wana ushahidi juu ya matumizi ya kemikali hiyo ya sumu iliyotumiwa na Ukraine, japo hakutoa maelezo ya kina kuhusu ushahidi huo.

Hata hivyo, hakukuwa na tamko kutoka upande wa Ukraine ambayo nayo imeituhumu Urusi kwa kutumia kemikali hiyo ya sumu.

Wakati huo huo, Urusi imesema itajibu vikwazo iliyowekewa na Umoja wa Ulaya ambavyo Moscow inavichukulia kuwa hatari kwa usalama wa nishati duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW