1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaadhimisha kuyanyakua majimbo ya Ukraine kwa tamasha

29 Septemba 2023

Urusi leo inadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu iliponyakua kinyume cha sheria majimbo manne ya mashariki na kusini mwa Ukraine.

Luhansk
Urusi imekuwa ikifanya ukarabati mkubwa kwenye majimbo ya Kherson, Zaporizhzhia, Donetsk na Luhansk tangu ilipoyanyakuwa mwaka mmoja uliopita. Mfano ni kituo hicho kipya cha vijana kwenye mkoa wa Luhansk.Picha: Alexander Reka/TASS/dpa/picture alliance

Kumbukumbu hiyo inaambatana na tamasha litakalofanyika katika uwanja wa kihistoria wa Red Square, mjini Moscow, ambalo linalenga kuutambulisha umma likizo mpya itakayokuwa ikiadhimishwa nchini humo.

Hata hivyo, vikosi vya Urusi havidhibiti kikamilifu majimbo ya Kherson, Zaporizhzhia, Donetsk na Luhansk, na imelazimika wakati mwingine kusalimisha maeneo kadhaa kufuatia mashambulizi ya Ukraine.

Wakati huo huo, makabiliano baina ya Urusi na Ukraine yameendelea kuripotiwa sehemu mbalimbali. Idara ya ulinzi wa anga ya Moscow imesema imeziharibu ndege 11 zisizo na rubani zilizorushwa na Ukraine katika maeneo ya Kursk na katika mkoa wa Kaluga takriban kilomita 200 kusini-magharibi mwa Moscow.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW