1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaahidi msaada wa kijeshi Afrika Magharibi

8 Februari 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ameahidi msaada wa nchi yake kwa nchi za Afrika Magharibi katika mapambano dhidi ya makundi ya itikadi kali.

Minister Sergey Lavrov trifft  Esteban Lazo Hernandez
Picha: Russian Foreign Ministry Press Service/AP/picture alliance

Lavrov ametoa ahadi hiyo akiwa katika ziara yake ya kwanza nchini Mali, ambapo amesifu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili alioutaja kuwa wa kihistoria. Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Urusi amesema msaada huo utazifikia pia nchi nyingine za ukanda huo, zikiwemo Guinea, Burkina Faso na Chad.

Miaka iliyopita Mali ilitegemea mkoloni wake wa zamani, Ufaransa, kwa msaada wa kijeshi katika kukabiliana na waasi, lakini Ufaransa iliwaondoa wanajeshi wake kutoka Mali mwaka uliopita baada ya kutokea mgongano baina yake na watawala wa kijeshi waliochukua madaraka mjini Bamako.

Tangu kushika hatamu za uongozi, wanajeshi hao wamepata msaada wa silaha na wakufunzi wa kijeshi kutoka Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW