1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yaangusha makombora yaliyorushwa kwenye mikoa yake

Sylvia Mwehozi
9 Julai 2023

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi imeangusha makombora manne siku ya Jumapili, mojawapo katika Rasi iliyonyakuliwa ya Crimea na matatu yameangushwa kwenye mkoa wa Urusi wa Rostov na Bryansk unaopakana na Ukraine.

Ukraine, Urusi
Askari wa Urusi akikagua kipande cha roketi la UkrainePicha: Alexander Polegenko/Tass/picture alliance

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi imeangusha makombora manne siku ya Jumapili, mojawapo katika Rasi iliyonyakuliwa ya Crimea na matatu yameangushwa kwenye mkoa wa Urusi wa Rostov na Bryansk unaopakana na Ukraine.

Gavana wa Crimea Sergei Aksyonov aliandika kupitia mtandao wa Telegram akisema kuwa kombora moja limeangushwa karibu na mji wa Kerch kwenye rasi hiyo ingawa hakubainisha limerushwa kutoka wapi.Urusi yaongeza mashambulio yake dhidi ya Ukraine

Maafisa wa eneo hilo wamesema shughuli kwenye daraja la Crimea linalounganisha Rasi ya Crimea na Urusi bara, zimerejeshwa baada ya kusimamishwa kwa muda.

Crimea ilinyakuliwa na Urusi kutoka Ukraine mnamo mwaka 2014, lakini imeendelea kutambuliwa kimataifa kama sehemu ya Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW