Urusi yaanza kupeleka nishati ya nyuklia Iran
17 Desemba 2007Matangazo
Urusi imeanza kupeleka nishati ya nyuklia katika kinu cha Beshehr nchini Iran. Marekani na mataifa ya Umoja wa Ulaya yanashuku Iran inapania kutengeneza silaha za nyuklia na yameitaka Urusi iache ushirikiano wake katika mradi wa Bushehr.
Iran inasema mpango wake wa nyuklia ni wa matumizi ya amani na imekataa kusitisha urutubishaji wa madini ya uranium.
Ujenzi wa kinu cha Bushehr umekuwa ukicheleweshwa huku Urusi ikisingizia mizozo ya malipo ya fedha kama sababu. Urusi inasema mivutano hii sasa imetatuliwa.