1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yaanzisha tena mashambulizi dhidi ya Ukraine

Saleh Mwanamilongo
21 Aprili 2025

Jeshi la Urusi limesema Jumatatu (21.04.2025) kuwa imeanzisha tena mashambulizi dhidi ya Ukraine baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na sikukuu ya Pasaka.

Wanajeshi wa Ukraine wakifanya mazoezi ya uokoaji karibu na uwanja wa vita
Wanajeshi wa Ukraine wakifanya mazoezi ya uokoaji karibu na uwanja wa vitaPicha: Yan Boechat/DW

Hata hivyo pande zote mbili zimeshtumiana kukiuka usitishwaji huo wa mapigano kwa saa 30, Ukraine ikisema Urusi ilishambulia kwa droni na makombora maeneo ya Dnipropetrovsk na Mykolaiv.

Hata hivyo Moscow imekanusha taarifa hiyo na kueleza kuwa vikosi vyake viliheshimu kikamilifu hatua hiyo iliyochukuliwa na rais Vladimir Putin.

Aidha, Msemaji wa wizara ya mambo ya Nje wa China Guo Jiankun amepongeza juhudi zote zinazo chukuliwa ili kufikia usitishaji mapigano nchini Ukraine, akisisitiza kuwa ni hatua muhimu kuelekea amani.