1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaapa kujibu vitisho kwenye mpaka wake wa Magharibi

9 Agosti 2023

Moscow imezishutumu Poland na Finland kwa kutishia usalama wake na kuapa kujibu vitisho vinavyozidi kuongezeka kwenye mipaka ya Urusi ya upande wa magharibi kutoka kwa wanachama wa Jumuiya ya kujihami, NATO.

Ukraine-Krieg | Russischer Panzer bei Isjum
Picha: Juan Barreto/AFP

Waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu amesema leo kwenye mkutano na maafisa wa kijeshi kwamba vitisho kwa usalama wa kijeshi wa Shirikisho la Urusi vimeongezeka katika maeneo ya kimkakati ya magharibi na kaskazini magharibi na kuongeza kuwa hatua hiyo inahitaji majibu yanayofaa.

Poland, mshirika mkubwa na jirani wa Ukraine imeimarisha usalama kwenye mipaka yake na Belarus baada ya Minsk kuwa makao mapya ya wapiganaji wa kundi la Wagner.

Finland inayopakana na Urusi, ilijiunga na NATO mwezi Aprili katika hatua ya kihistoria iliyochochewa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Katika hatua nyingine, Warsaw imetangaza itapeleka wanajeshi 2,000 zaidi kwenye mpaka wake wa mashariki kuungana na wanajeshi wengine 2,000 walioko kwenye eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW