Urusi yachukuwa udhibiti wa maeneo mawili ya makazi Ukraine
19 Januari 2026
Ripoti hiyo ya Urusi ya kuteka maeneo mawili ya Ukraine haikuweza kuthibitishwa na Reuters kwa njia huru.
Urusi yashambulia kituo cha miundo mbinu Kharkhiv
Meya wa Kharkiv Ihor Terekhov, amesema leo kuwa kituo kimoja muhimu cha miundombinu kimeharibiwa mjini humo kutokana na shambulizi la Urusi.
Kwenye ujumbe katika mtandao wa Telegram, Terekhov amesema adui alishambulia kituo hicho kwa makombora kadhaa na kusababisha uharibifu mkubwa. Hata hivyo hakutoa maelezo yoyote kuhusu aina ya kituo kilichoshambuliwa.
Katika hatua nyingine, wafanyakazi wa ukarabati wa dharura wanafanya kazi kwa bidii ili kurejesha nguvu za umeme mkoani Kyiv nchini Ukraine, baada ya mfululizo wa mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundombinu ya nishati kuwaacha raia wa eneo hilo kwenye kibaridi kikali cha msimu wa huu wa baridi.