1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yadai kuzuia ndege za kivita za Marekani

21 Julai 2024

Urusi imedai kwamba ilituma ndege zake za kivita za kwenda kuzizuia ndege mbili za kijeshi za Marekani zilizojaribu kuvuka mpaka wake kwenye Bahari ya Barents iliyo katika kanda ya Aktiki.

Ukraine | Charkiw
Urusi imedai kwamba ilituma ndege zake za kivita za kwenda kuzizuia ndege za kijeshi za Marekani.Picha: Inna Varenytsia/REUTERS

Jeshi la Marekani mara kwa mara hufanya operesheni za ndege juu ya eneo la maji ya kimataifa, ambazo inasema ni halali kufanywa katika anga ya upande wowote na kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Hata hivyo Moscow imejibu kwa ukali operesheni hizo katika katika miezi ya hivi karibuni, na mwezi Juni ilionya kwamba ndege zisizo na rubani za Marekani juu ya Bahari Nyeusi zinatishia kuzusha makabiliano ya "ya moja kwa moja" ya kijeshi.

Moscow imekuwa ikiishutumu Marekani kwa kutumia ndege zake zisizo na rubani zinazofanya ujasusi juu ya maji yasiyo na upande wowote katika Bahari Nyeusi ili kuisaidia Ukraine kushambulia rasi ya Crimea inayoshikiliwa na Urusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW