1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yadai kuzuia shambulio kubwa la droni 20 za Ukraine

26 Novemba 2023

Urusi imesema leo kuwa imezuia shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani za Ukraine huku takriban Droni 20 zikidunguliwa katika mikoa ya Urusi, ikiwemo Moscow

Maafisa wa zima moto wa Ukraine wanajizatiti kuzima moto kufuatia shambulizi la usiku kucha la ndege zisizo na rubani za Urusi mnamo Novemba 3 2023
Maafisa wa zima moto wa Ukraine wanajizatiti kuzima moto kufuatia shambulizi la usiku kucha la ndege zisizo na rubani za Urusi Picha: Titov Yehven/abaca/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema ndege zisizo na rubani za Ukraine zilidunguliwa katika maeneo ya Tula, Kaluga na Bryansk. Gavana wa mkoa wa Tula Alexei Dyumin, amesema mtu mmoja amejeruhiwa wakati ndege moja ilipogonga jengo la ghorofa.

Soma pia:Mashambulizi nchini Urusi yaharibu dhana ya 'jeshi la Putin'

Gazeti la  kila siku la nchini Urusi Kommersant, limeripoti kuwa safari za ndege zimecheleweshwa ama kufutiliwa mbali katika viwanja vikubwa vya ndege mjini Moscow kutokana na shambulizi hilo .

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW