1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yadungua droni 126 za Ukraine

Hawa Bihoga
29 Septemba 2024

Urusi imesema imedungua droni 125 za Ukraine zilizovurumkishwa usiku kucha huku jengo la makaazi ya raia lilishambuliwa katika mji wa magharibi wa Voronezh.

Ukraine | Jengo la makaazi liharibiwa kwa mashambulizi.
Jengo likiwa limeharibika kutokana na mashambulizi kati ya Urusi na UkrainePicha: National Police of Ukraine in Sumy region/REUTERS

Wizara ya Ulinzi Urusi imesema mashambulizi ya hivi karibuni yalilenga eneo la kusini la Volgogran ambapo droni 67 zilidunguliwa na  nyingine 17 ziliangushwa katika mikoa ya Belgorod na Voronezh huku 18 zilidunguliwa katika eneo la Rostov.

Ama kwa upande mwingine Gavana wa mkoa wa Belgorod Vyacheslav Gladkov ameripoti kwamba mtu mmoja ameuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa katika mkururo wa mashambulizi ya Ukraine ya makombora na droni kwa saa 24 zilizopita.

Soma pia:Mashambulizi ya Urusi katika hospitali Ukraine yaua watu saba

Vikosi vya Urusi vinaposonga mbele kwenye uwanja wa vita mashariki mwa Ukraine, Kyiv nayo imekuwa ikifanya mashambulio ya kuvuka mpaka katika eneo la Kursk magharibi mwa Urusi tangu Agosti 6 na kuendeleza mashambulizi makubwa ndani ya ardhi ya Urusi.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW