1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yadungua droni mbili za Ukraine

10 Agosti 2023

Maafisa nchini Urusi wamesema leo kwamba wamezidungua ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine zilizokuwa zinaelekea Moscow.

Afghanistan Kandahar | Sicherheit | Indien untersagt Verwendung von Drohnen aus China
Ndege isiyokuwa na rubaniPicha: Efren Lopez/U.S. Air Force photo/REUTERS

Maafisa nchini Urusi wamesema leo kwamba wamezidungua ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine zilizokuwa zinaelekea Moscow, ikiwa ni siku ya pili mfululizo ya mashambulizi yanayovuruga safari za ndege kwenye viwanja viwili vya ndege vya kimataifa, wakati Ukraine ikiongeza mashambulizi katika ardhi ya Urusi.

Meya wa Moscow Sergey Sobyanin na wizara ya ulinzi ya Urusi, zimeeleza kuwa ndege moja isiyo na rubani iliangushwa karibu na eneo la Kaluga, kusini magharibi mwa Moscow na nyingine karibu na barabara kubwa ya mzunguko mjini Moscow,

Hata hivyo, hakukua na majeruhi na haikuwa wazi ndege hizo zilirushwa kutokea eneo gani.

Maafisa wa Ukraine hawakusema lolote kuhusiana na kisa hicho na mara nyingi imekuwa haikiri wala kukanusha kufanya mashambulizi kama hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW