1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yadungua droni tisa za Ukraine karibu na Moscow

14 Desemba 2023

Urusi imesema leo kwamba mifumo yake ya ulinzi wa anga imeangusha ndege tisa za Ukraine zisizo na rubani zilizokuwa zikielekea katika mji wake mkuu Moscow.

Ukraine | Askari jeshi wa Ukraine akiwa katika uwanja wa vita eneo la Donetsk.
Mwanajeshi wa Ukraine katika kikosi cha ardhini akiwa katika uwanja wa mapambano huko DonetskPicha: Ozge Elif Kizil/AA/picture alliance

Shambulizi hilo lililoripotiwa, lilitokea saa chache kabla ya rais wa nchi hiyo Vladmir Putin kufanya mkutano wake wa kwanza na wa mwisho wa mwaka na wanahabari tangu kuanzisha mashambulizi nchini Ukraine mwezi Februari 2022, na siku moja baada ya shambulio la kombora la Urusi kujeruhi mamia ya watu mjini Kyiv.

Soma pia:Urusi yarusha makombora, droni 23 kuelekea Ukraine

Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Urusi, imesema kuwa vitengo vya ulinzi wa anga vilivyokuwa vikishika doria viliharibu na kunasa ndege hizo tisa zisizo na rubani katika maeneo ya Kaluga na Moscow na kuilamu Ukraine kwa shambulizi hilo.

Meya wa  Moscow Sergei Sobyanin amesema ndege moja ililengwa na kuangushwa karibu na Naro-Fominsk, mji ulioko Kusini Magharibi mwa Moscow.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW