1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yaendeleza mashambulizi katika mji wa Kharkiv

24 Septemba 2024

Urusi imelenga jengo moja la ghorofa katika mji wa kaskazini mashariki wa Kharkhiv leo, wakati wa mashambulizi ya makombora ya kuongozwa, na kuwauwa takriban watu watatu na kuwajeruhi zaidi ya 22.

Mashambulizi ya Urusi mjini Kharkiv
Mashambulizi ya Urusi mjini KharkivPicha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Urusi imelenga jengo moja la ghorofa katika mji wa kaskazini mashariki wa Kharkhiv leo,  wakati wa mashambulizi ya makombora ya kuongozwa, na kuwauwa takriban watu watatu na kuwajeruhi zaidi ya 22 huku wengine wakihofiwa kukwama chini ya vifusi.

Haya ni kwa mujibu wa mamlaka ya eneo hilo.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegraph, afisa wa kuchunguza malalamishi dhidi ya maafisa wa serikali wa Ukraine Dmytro Lubinets, amesema Urusi inalishambulia eneo la Kharkiv bila kujali sheria kwa mashambulizi ya moja kwa moja kwenye majengo ya makazi.Rais Volodymyr Zelensky afanya ziara katika jimbo la Kharkiv

Katika ujumbe wa Telegram, meya wa Kharkiv Ihor Terekhov alisema kuwa jengo hilo tayari lilikuwa limeshambuliwa na Urusi mwanzoni mwa uvamizi wake kamili nchini Ukraine mnamo mwaka 2022 na kuanza kufanyiwa marekebisho, lakini adui amelilenga kwa mara ya pili.

Terekhov ameongeza kuwa Urusi imeshambulia takriban wilaya nne leo alasiri ikiwa ni pamoja na eneo lenye idadi kubwa ya watu mjini humo.