1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaendeleza mashambulizi katika mkoa wa Donetsk

9 Desemba 2022

Watu watano wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia mashambulizi mabaya ya Urusi katika eneo la Donetsk

Ukraine-Krieg I Bakhmut
Picha: LIBKOS/AP/picture alliance

Gavana wa mkoa wa Donetsk Pavlo Kyurilenko amesema mapigano makali yaliripotiwa karibu na miji ya Bakhmut na Avdiivka na kwamba vikosi vya Urusi vilijaribu kusonga mbele karibu na Lyman, ambayo ilidhibitiwa tena na vikosi vya Ukraine mwezi Novemba.

Hayo yanajiri wakati jana Marekani na Urusi walifikia hatua ya kubadilishana wafungwa ambapo Urusi ilimuachia huru mchezaji wa mpira wa kikapu Brittney Griner huku Marekani ikimuachia muuzaji wa silaha, Viktor Bout.

Ikulu ya White House imesema ubadilishanaji huo wa wafungwa hautaathiri azma ya Marekani kwa watu wa Ukraine. Jana, Bunge la Marekani lilipitisha muswada wa sheria wa kuipatia mwakani Ukraine dola milioni 800 za zaida katika mpango wake wa usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW