1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaendeleza Mashambulizi Ukraine

Bakari Ubena17 Machi 2022

Wakati bado jumuia za kimataifa zinaendelea kuisaka suluhu kuumaliza mzozo wa Urusi na Ukraine,Urusi imeendeleza mashambulizi yake katika maeneo muhimu ya Ukraine

Ukraine Charkiw | Zerstörtes Wohngebäude nach Beschuss
Picha: Pavel Dorogoy/AP Photo/picture alliance

Urusi ilitarajia kushinda vita hivyo ndani ya siku chache lakini vimeingia wiki yake ya nne na wakati huohuo mazungumzo ya kutafuta suluhu kwa njia za za kidiplomasia yakiendelea.

Maafa yanaripotiwa sehemu mbalimbali nchini Ukraine lakini Mariupol imekumbwa na janga baya zaidi la kibinadamu katika vita hivi, huku mamia kwa maelfu ya raia wakijificha kwenye handaki bila chakula, maji au umeme kwa wiki kadhaa sasa.

Soma zaidi:Zelensky aitaka Ujerumani kuuvunja ukuta wa Urusi

Wiki hii, vikosi vya Urusi vimeanza kuruhusu baadhi ya watu kuondoka eneo hilo kwa kutumia magari yao binafsi lakini wameizuia misafara ya misaada kufika mjini.

UN:zaondi ya watu 700 wamefariki katika mashambulizi hayo

Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet,amesema watu 780 wameuawa nchini Ukraine tangu wanajeshi wa Urusi walipoivamia kijeshi Ukraine wiki tatu zilizopita, wakiwemo watoto 58 miongoni mwa wahasiriwa.

Michelle Bachelet Kamishna mkuu wa haki za binadamu Umoja wa MataifaPicha: Wang Ying/Xinhua News Agency/picture alliance

Ofisi hiyo imesema leo Alhamisi kuwa imethibitisha pia habari kuhusu watu 1,252 ambao wamejeruhiwa. Michelle Bachelet, amesisitiza kuwa idadi halisi huenda ikawa juu zaidi

Soma zaidi:Rais Joe Biden amwita Putin kuwa mhalifu wa kivita

Ingawa pande zote mbili katika mzozo huu zimeashiria maendeleo madogo katika mazungumzo ya amani wiki hii, Rais Vladimir Putin, ambaye aliamuru uvamizi wa Urusi mnamo Februari 24, haonyeshi dalili japo ndogo za kupunguza mashambulizi.

Mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine yanaendelea kwa njia ya video. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova amesema wajumbe hao wanajadili masuala ya kijeshi, kisiasa na kibinadamu na kwamba ombi la Urusi liko wazi.

Zakharova alisema kuwa madai ya Urusi yapo wazi na ndio yaliosababisha kuwepo kwa kile alichokiita Oparesheni maalum ya kijeshi "Tunatumai  Kyiv wametambua jambo lisiloepukika la kuachana na upanuzi wa kijeshi." Aliwaambia waandishi wa habari.

Aliongeza kuwa tumaini la Urusi ni Ukraine kuwa nchi huru isioegemea upande wowote kwa manufaa ya watu wa Ukraine na ulaya kwa ujumla wake.

Marekani kufanya mazungumzo bna China

Rais wa Marekani Joe Biden atafanya mazungumzo kwa njia ya simu na kiongozi wa China Xi Jinping kesho Ijumaa ili kujadili vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na masuala mengine yanayohusu pande zote.

Bendera za China na MarekaniPicha: Dwi Anoraganingrum/Geisler-Fotopress/picture alliance

Serikali za Ulaya zinaielekea Marekani na makampuni ya ulinzi  huku zikiwa na orodha ya ununuzi wa silaha ikiwa ni pamoja na ndege zisizo na rubani na makombora ya kujihami. Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unafufua upya mahitaji ya silaha za Marekani.

soma zaidi:Zelenskiy kulihutubia bunge la Marekani

Dmitry Medvedev, naibu mkuu wa baraza la usalama la Putin, amesema Marekani imechochea kauli za chuki dhidi ya Urusi katika kujaribu bila mafaaniko kuilazimisha Urusi kutii amri. Medvedev amesema Urusi ina uwezo wa kupambana vilivyo na maadui zake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW