1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kyiv: Urusi yafanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani

Hawa Bihoga
24 Desemba 2023

Urusi imeendeleza mkururo wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani usiku kucha, huku ndege 14 kati ya 15 zikidunguliwa na jeshi la anga la Ukraine.

Ukraine | Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani
Polisi wakilichunguza jengo lililoharibiwa na shambulio la ndege za Urusi zisizokuwa na rubani mjini KyivPicha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Mikoa ambayo imeathirika na mashambulizi hayo ni pamoja na Mykolaiv, Zaporizhzhya na Dnipropetrovsk.

Mashambulizi hayo yanafanyika wakati Ukraine ikijiandaa kusherehekea sikukuu ya Krismasi ya Orthodox, ambayo Ukraine ikiihamisha kutoka Januari 7 hadi Desemba 25, kufuatia uvamizi wa jirani yake Urusi ulioanza takriban miaka miwili iliopita.

Mamlaka ya Ukraine pia imeripoti majeruhi na vifo katika eneo la Kusini la Kherson kufuatia mashambulizi ya Urusi.

Mamlaka imeeleza kuwa mashambulizi ya Urusi yamesababisha vifo vya watu wanne na wengine tisa wamejeruhiwa huku mtoto mmoja akiwa miongoni mwa majeruhi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW