1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yafanya mashambulio ya Droni katika mji wa Odessa

4 Septemba 2023

Vikosi vya Ukraine vimezidungua ndege 17 zisizoendeshwa na rubani za Urusi katika anga ya eneo la Kusini la Odesa.

Ukraine Krieg Raketenagriff auf Odessa
Sehemu ya kituo cha manunuzi kilichoshambuliwa Odessa, UkrainePicha: Nina Liashonok/REUTERS

Taarifa hiyo imeelezwa na gavana wa eneo hilo Oleg Kiper, leo Jumatatu,akisema mashambulizi hayo yamesababisha uharibifu katika wilaya iliyoko katika mto Danube inayopakana na nchi ya  Romania.

Kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa Telegram gavana Kiper amesema wanajeshi wa kikosi cha ulinzicha Ukraine walizidungua ndege hizo lakini pia kwa bahati mbaya kuna mashambulizi yaliyoharibu majengo ya maghala,majengo ya shughuli za uzalishaji bidhaa,pembejeo za kilimo na vifaa vingine vya viwandani katika wilaya ya Izmail.

Soma pia:Droni za Urusi zaushambulia mji wa Odesa kwa saa tatu

Wakati huohuo rais Volodymr Zelensky Jana alitangaza mabadiliko kwa kumuondowa waziri wa ulinzi Oleksiy Reznikov na kutowa mwito wa kuwepo mwelekeo mpya, mwaka mmoja na nusu tangu uvamizi wa Urusi.

Tangazo la rais Zelensky lilitolewa saa chache baada ya Ukraine kushuhudia mashambulizi hayo ya droni katika eneo la Odesa.