1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yafanya mashambulizi 114 Ukraine ndani ya masaa 24

11 Oktoba 2024

Vikosi vya jeshi la Urusi vimefanya mashambulizi 114 kwenye eneo la mashariki mwa Ukraine ndani ya masaa 24 yaliyopita.

Ukraine Urusi
Moshi ukifuka baada ya mashambulizi ya Urusi kwenye mkoa wa Donetsk.Picha: Thomas Peter/REUTERS

Kwa mujibu wa jeshi la Ukraine, mashambulizi, mashambulizi 30 yamefanyika kwenye mstari wa mbele wa mapambano wa Lyman, njia ya reli iliyoko kwenye mkoa wa Donetsk. Maeneo mengine yaliyoshambuliwa ni Pokrovsk na Kurakhiv.

Blogu isiyo rasmi ya masuala ya kijeshi ya Ukraine, DeepState, iliripoti hapo jana kuwa miji minne midogo mashariki mwa nchi hiyo imeangukia mikononi mwa jeshi la Urusi.

Soma zaidi: Zelensky awasilisha "mpango wa ushindi" wa vita na Urusi

Hayo yanakuja wakati idadi ya waliouawa kwenye mashambulizi ya jana ya makomora ya Urusi katika mji wa pwani wa Odessa, ikifikia watu wanane.

Gavana wa kijeshi wa eneo hilo, Oleh Kiper, ameandika kupitia mtandao wa Telegram kwamba kijana wa miaka 26 aliyejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo, amefariki dunia akiwa hospitalini. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW