1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yafanya mashambulizi katika mji wa Lviv Ukraine

4 Septemba 2024

Urusi imefanya mashambulizi dhidi ya mji wa Lviv, ulioko magharibi mwa Ukraine leo na kusababisha vifo vya watu 7 na kuharibu majengo kadhaa ya kihistoria katika shambulio hilo la nadra.

Ukraine | Shambulio la Urusi likiharibi miundombino
Shambulio la Urusi lililoharibu moja ya majengo ya UkrainePicha: Roman Baluk/REUTERS

Urusi imeimarisha mashambulizi dhidi ya Ukraine tangu Kiev ilipoanzisha operesheni ya kuvuka mpaka na kuingia katika jimbo la Kursk mwezi uliopita.

Soma pia: Mashambulizi ya Urusi yauwa 7 Lviv

Miongoni mwa waliouwawa Lviv ni pamoja na watoto watatu. Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Igor Klymenko kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa wa Telegram, amesema operesheni ya uokoaji na kutafuta manusura inaendelea.

Watu 40 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW