MigogoroUlaya
Urusi yafanya mashambulizi makubwa nchini Ukraine
27 Aprili 2024Matangazo
Taarifa hii ni kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo. Jeshi la Ukraine limesema Urusi ilifyetua makombora 34 ambapo 21 kati yao yalidunguliwa.
Waziri wa nishati wa nchi hiyo German Galushchenko amesema mashambulizi hayo yamelenga vituo vya nishati katika maeneo matatu huku kampuni moja kubwa ya kutengeneza umeme DTEK ikiongeza kuwa mitambo yake minne ya kufua umeme pia imeharibiwa vibaya.
Katika ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Galushchenko amesema kuwa kwa mara nyingine tena, adui amelenga miundo mbinu ya nishati hasa katika maeneo ya Dnipropetrovsk, Ivano-Frankivsk, na Lviv.