1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yafanya mashambulizi makubwa mjini Kyiv

25 Novemba 2023

Maafisa wa Ukraine wamesema Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani yalioulenga mji mkuu Kyiv ambayo hayajawahi kushuhudiwa tangu Moscow ilipoanzisha uvamizi wake February mwaka 2022.

Ukraine | Zerstörung in Kiev
Maafisa wa Polisi wa Ukraine wakikagua jumba la kuwapokea watoto lililoshambuliwa na makombora ya Urusi mjini Kyiv: 25.11.2023Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Mashambulizi hayo yamepeleka watu watano kuuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema jeshi lake la anga limedungua ndege zisizo na rubani zaidi ya 70 aina ya Shahed zilizotengenezwa na Iran na kurushwa na vikosi vya Moscow.

Zelenskiy amesisitiza kuwa mashambulizi hayo yamejiri wakati Ukraine ikiadhimisha janga lisilosameheka la Holodomor ambapo kati ya mwaka 1932-1933, mamilioni ya wa Ukraine walikufa kwa njaa kutokana na hatua kali za Joseph Staline, kiongozi wa wakati huo wa Umoja wa Kisovieti.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW