Urusi yafanya mashambulizi makubwa nchini Ukraine
20 Septemba 2025
Matangazo
Katika taarifa kupitia mtandao wake rasmi wa Telegram, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, amesema mashambulizi hayo yamefanyika katika mikoa tisa ikiwa ni pamoja na Dnipropetrovsk, Mykolaiv, Chernihiv, Zaporizhzhia, Poltava, Kyiv, Odesa, Sumy na Kharkiv.
Rais huyo amesema lengo la kile alichokiita adui ni miundombinu yao, maeneo ya makazi na makampuni ya kibiashara ya raia.
Pia amesema kombora moja lililenga jengo la ghorofa nyingi katika jiji la Dnipro.
Rais Zelensky ameongeza kuwa kila shambulizi sio shabaa ya kijeshi lakini ni mkakati wa makusudi wa Urusi kuwatisha raia na kuharibu miundombinu yao.