1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yafanya mashambulizi makubwa nchini Ukraine

18 Mei 2026

Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya anga na kuilenga mikoa kadhaa nchini Ukraine ikiwa ni pamoja na Dnipro, ambapo raia zaidi ya 20 wakiwemo watoto watatu wamejeruhiwa.

Dnipro | Urusi yafanya mashambulizi makubwa nchini Ukraine
Vikosi vya zimamoto huko Dnipro baada ya mashambulizi ya UrusiPicha: REUTERS

Hayo yameelezwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na kuongeza kuwa Urusi ilifyetua jumla ya makombora 22 ya masafa na droni 524.

Kwa siku kadhaa sasa, Moscow imekuwa ikijibu mashambulizi makubwa zaidi ya droni yaliyofanywa na Ukraine na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wanne, wakiwemo watatu karibu na Moscow. Wiki iliyopita, shambulio la Urusi lilibomoa jengo la ghorofa mjini Kyiv ambapo watu 24 waliuawa.

Hadi sasa ,  hakuna ishara ya kufikiwa kwa makubaliano ya amani  licha ya juhudi za kidiplomasia zinazoongozwa na Marekani kujaribu kukomesha uvamizi huo. Hayo yanaripotiwa wakati rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kuanza hapo kesho ziara yake nchini China na anatarajiwa kukutana na mwenzake Xi Jinping, ikiwa ni siku chache baada ya ziara ya rais wa Marekani Donald Trump mjini Beijing.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW