Urusi yafanya mazoezi ya kijeshi katika Bahari Nyeusi
21 Julai 2023Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema mazoezi hayo ya jeshi la wanamaji ni hatua ya kuziba baadhi ya njia katika Bahari Nyeusi ambayo inatumika kusafirisha nafaka kutoka Ukraine.
Zoezi hilo limekuja baada ya Moscow kutangaza maeneo makubwa ya Bahari Nyeusi kuwa ni hatari kwa urambazaji kufuatia kujiondoa katika mpango huo wa nafaka.
Soma pia:Urusi na China zafanya luteka za pamoja za kijeshi
Katika taarifa yake wizara hiyo imethibitishwa kwamba, boti ya Moscow ilifyatua moja kwa moja makombora ya kuzuia meli katika meli iliolengwa huko kaskazini magharibi mwa Bahari Nyeusi, na meli hiyo iliharibiwa vibaya kutokana na shambulio la kombora.
Mmoja wa wahudumu katika kikosi hicho cha wanamaji cha Moscow amesema, katika mazoezi ya leo, mashua mbili zilifanya shambulio la meliya adui wa kubuni.
"Mazoezi ya mapigano yalifanyika kwa kutumia silaha za kombora."
Alisema wakati mazoezi ya kijeshi yakiendelea na kuongeza kwamba katika ufyatuaji wa makombora ulifanikiwa, adui wa kubuni aliangamizwa.
Soma pia:Urusi yazitahadharisha meli zinazotumia njia ya Bahari Nyeusi
Baada ya kujiondoa katika makubaliano ya kuwezesha usafirishaji salama wa nafaka kutoka Ukraine, Kremlin ilisema Jumatano kwamba, itazizingatia meli za mizigo zinazopelekwa Ukrainekupitia Bahari Nyeusi.
Kadhalika katika taarifa yake ilipiga marufuku shughuli za usafirishaji katika maeneo ya kaskazini magharibi na kusini mashariki mwa bahari.
Ukraine yasisitiza kuendelea kwa usafirishaji nafaka
Ukraine pia ilipiga marufuku urambazaji kwenye sehemu ya kaskazini-mashariki ya Bahari Nyeusi na Mlango-Bahari wa Kerch karibu na Crimea, na kufanya urambazaji katika sehemu kubwa ya Bahari Nyeusi kuwa hatari kwa meli.
Ukraine imeendelea kusisitiza kwamba itakuwa tayari kuendelea na mauzo ya nafaka kutoka bandari zake za kusini kufuatia Moscow kujiondoa katika makubaliano hayo.
Imetoa wito pia kwa Umoja wa Mataifa na nchi jiranikuwekwa kwa njia salama kwa mizigo kupitia doria za pamoja.
Zelenskiy amfuta kazi Balozi wake wa Uingereza
Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine amemfuta kazi Vadym Prystaiko kama balozi wa Ukraine nchini Uingereza leo Ijumaa, ikiwa ni siku chache baada ya mwakilishi huyo kumkosoa rais hadharani.
Amri ya rais, ambayo ilisema Prystaiko pia ameondolewa kama mwakilishi wa Ukraine katika Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini, haikutoa sababu ya kufutwa kazi.
Soma pia:Zelensky amfuta kazi balozi wake nchini Uingereza
Katika mahojiano na shirika la habari la Sky wiki iliyopita, Prystaiko aliulizwa kuhusu matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Uingereza anayemaliza muda wake Ben Wallace.
Mwanadiplomasia huyo, alipendekeza Kyiv ionyeshe shukrani zaidi kwa uwasilishaji wa silaha kutoka kwa washirika wake ili kupambana na vikosi vinavyoikalia kwa mabavu vya Urusi.
Agizo la Zelensky halikusema wazi ni naniangelichukua nafasi ya mwanadiplomasia huyo mzoefu na makamu waziri mkuu wa zamani ambaye, alishikilia wadhifa huo kama balozi nchini Uingereza kwa miaka mitatu.