1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yafanya shambulizi dhidi ya gridi ya umeme ya Ukraine

20 Januari 2026

Urusi imeishambulia Ukraine kwa zaidi ya droni 300 na makombora katika shambulizi la usiku kwenye gridi yake ya umeme.

Ukraine Kyiv 2026 | mashambulizi a Urusi
Shambulizi la Urusi nchini Ukraine mnamo Januari 20, 2026Picha: Gleb Garanich/REUTERS

Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko amesema shambulizi hilo lilisababisha kukatika kwa umeme katika zaidi ya majengo  5,600 ya ghorofa kwenye mji huo mkuu.

Takriban asilimia 80 ya majengo yaliyoathiriwa yalikuwa yamerejeshewa umeme hivi karibuni baada ya shambulizi kubwa la Urusi mnamo Januari 9 lililowaathiri maelfu ya watu kwa siku kadhaa.

Wakati huo huo, maafisa wa Ukraine wanajaribu kuendeleza kasi ya mazungumzo ya amani yanayoongozwa na Marekani. Timu yake ya mazungumzo iliwasili Marekani siku ya Jumamosi. Kwa mujibu wa Zelensky, jukumu lake kuu ni kueleza jinsi mashambulizi ya Urusi yanahujumu diplomasia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW