1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yafungia baadhi ya vyombo vya habari vya Ulaya

26 Juni 2024

Urusi imepiga marufuku vyombo 81 vya habari kutoka Umoja wa Ulaya kupeperusha matangazo yake ndani ya nchi hiyo ikiwemo shirika la habari la Ufaransa la AFP na Politico.

Urusi | Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Mikhail Metzel/REUTERS

Hatua hiyo ni sehemu ya kulipiza kisasi kwa hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Ulaya kuvipiga marufuku vyombo vya habari vya Urusi.

Maafisa wa Urusi wanasema idadi kubwa ya vyombo vya habari vya magharibi vinaeneza ripoti zisizo za kweli kuhusu kile Urusi inachosema ni oparesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine.

ICC yatoa waranti ya kukamatwa viongozi waandamizi wa Urusi

Marufuku hayo yanatokea baada ya Umoja wa Ulaya mnamo mwezi Mei kutangaza kuwa inaifunga kile walichokitaja kuwa mitandao minne ya propaganda inayohusishwa na Kremlin.

Umoja wa Ulaya ulieleza kuwa marufuku hiyo ililenga Sauti ya Ulaya, shirika la habari la RIA, na magazeti ya Izvestia na Rossiyskaya Gazeta.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW