1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yahamishia baadhi ya wanajeshi Dnipro, Ukraine

13 Novemba 2023

Urusi imesema inawahamishia baadhi ya wanajeshi wake katika maeneo waliyosema yatawafaa zaidi, mashariki mwa Mto Dnipro nchini Ukraine.

Baadhi ya wanajeshi wa Urusi
Baadhi ya wanajeshi wa Urusi Picha: Olga Maltseva/AFP

Mashirika ya habari la serikali ya RIA na TASS yameripoti taarifa yakinukuu wizara ya ulinzi ya Urusi na kusema majeshi yake yanajiunda upya mashariki mwa mto huo. 

Jeshi la Urusi lilisema siku ya Ijumaa kwamba vikosi vyake vimechukua hatua hiyo ili kuzuia jaribio la Ukraine la kutengeneza daraja jipya mashariki wa ukingo wa Mto Dnipro na visiwa vilivyo karibu na eneo hilo.

Zelensky ahofia mashambulizi ya Urusi ya msimu wa baridi

Hata hivyo shirika la habari la Reuters halikuweza kuithibitisha hilo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW