SiasaUkraine
Urusi yaiashambulia vikali Ukraine usiku wa kuamkia Ijumaa
10 Februari 2023Matangazo
Katika hatua za mapema takribani makombora 17 yamevurumishiwa katika mji wa kusini/mashariki wa taifa hilo wa Zaporizhzhia.
Gavana wa eneo la kusini mwa Ukraine la Udesa, Maksym Marchenko amesema kumekuwa na mashambulizi ya anga na meli za kivita zilizobeba makombora katika eneo la bahari.
Mashambulizi yamesababisha kelele za ving'ora vya tahadhari hadi asubuhi ya leo hatua ambayo imesababisha maafisa kuwataka raia kujihifadhi kwa hofu ya kutokea mashambulizi mengine zaidi.
Miundombinu muhimu pia imeshambuliwa katika mji wa Khmelnitskyi magharibi Ukraine, Kharkiv kaskazini mashariki na mkoa wa Dnipropetrovsk katikati mwa Ukraine.