1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaidungua droni ya Ukraine

28 Julai 2023

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema imeidungua ndege isiyokuwa na rubani ya Ukraine mapema leo nje kidogo ya mji mkuu, Moscow.

Ukraine Kiew | Rotes Kreuz
Mwakilishi wa Shirika la Msalaba Mwekundu akitembea karibu na magari yaliyoharibiwa na droni za Urusi.Picha: SOPA ImagesÆ/IMAGO/ZUMA Wire

Wizara hiyo imeeleza kwamba hakukuwepo majeruhi au uharibifu wowote kufuatia tukio hilo.

Hata hivyo, haikutoa maelezo juu ya sehemu ndege hiyo isiyo na rubani ilipodunguliwa, lakini imesema tukio hilo limefanyika katika eneo la Moscow Oblast, viungani mwa mji mkuu wa Moscow.

Jaribio hilo la shambulizi linaongeza wasiwasi juu ya uwezekano wa Moscow kushambuliwa katika wakati ambapo vita kati ya Urusi na Ukraine vinaingia mwezi wake wa 18.

Soma zaidi: Makombora kadhaa ya Urusi yarushwa Ukraine

Kulifanyika mashambulizi mawili ya ndege zisizokuwa na rubani mjini Moscow mnamo siku ya Jumatatu, moja likilenga katikati mwa mji huo karibu na makao makuu ya wizara ya ulinzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW