1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yailaumu Marekani kwa kuchochea vita vyake na Ukraine

3 Februari 2024

Baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Victoria Nuland kuzuru Ukraine, serikali ya Urusi inaishutumu Marekani kwa kile ilichoeleza kuchochea Kiev katika kuendeleza vita.

Victoria Nuland
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Victoria Nuland mjini KyivPicha: Roman Gritsyna/AP Photo/picture alliance

Baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Victoria Nuland kuzuru Ukraine, serikali ya Urusi inaishutumu Marekani kwa kile ilichoeleza kuchochea Kiev katika kuendeleza vita.

Kupitia televisheni ya umma, Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov ameonekana akisema "Wamarekani wanaongeza maumivu kwa watu wa Ukraine na wanasababisha vifo."

Soma: Ukraine yadai kuzidungua droni 9 kati ya 14 za Urusi

Amesema Marekani inahusika moja kwa moja katika mzozo huo na inazidi kujiingiza ndani zaidi, akisema hatua hiyo haiwezi kubadili mwelekeo wa vita vya Urusi na Ukraine.

Ikulu ya Kremlin daima inalaumu kuwa watu wengi wanaojeruhiwa katika vita ni kutokana kitendo cha nchi za Magharibi kusaidia Kiev katika kujinusuru na mashambulizi ya Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW