1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yaimarisha mzingiro dhidi ya Bakhmut

Daniel Gakuba
7 Machi 2023

Rais wa Ukraine amesema majenerali wa jeshi la nchi hiyo wameapa kuulinda mji wa Bakhmut wa mashariki mwa Ukraine, wakati ambapo wanajeshi wa Urusi wameimarisha mzingiro wao kwa lengo la kuukamata mji huo wa kimkakati.

Ukraine | Krieg | Zerstörung in Bachmut
Picha: Yevhen Titov/REUTERS

Urusi imekuwa ikijaribu kwa miezi kadhaa kuuteka mji huo, ikisema kuudhibiti kutakuwa ni hatua kubwa kuelekea kuushikilia ukanda mzima wa Donbas.

Hata hivyo, wapanga mikakati wa kimagharibi wanasema kuukamata mji wa Bakhmut hakutakuwa na uzito ikilinganishwa na gharama iliyolipa Urusi.

Wanajeshi wa Ukraine wameonekana kuimarisha ngome zao magharibi mwa Bakhmut katika kinachoaminika kuwa matayarisho ya kujiondoa, lakini bado haijawa bayana kama watafanya hivyo.

Rais Zelenskiy amesema amezungumza na makamanda wa kimkoa na wote wamesema hawauachi mji wa Bakhmut, bali wataimarisha ulinzi wao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW