1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yaishambulia mikoa 15 ya Ukraine

3 Oktoba 2024

Vikosi vya Urusi vimefanya mashambulizi ya droni katika mikoa 15 ya Urusi usiku wa kuamkia leo na kuharibifu katika maeneo ya biashara na majengo ya makaazi ya watu ingawa bado hakuna ripoti za majeruhi zilizoripotiwa

Ukraine | Jengo la makaazi likiwa limeharibiwa.
Mashambulizi ya Urusi yakiwa yameharibu jengo la makaazi Ukraine.Picha: Vitalii Hnidyi/REUTERS

Jeshi la wanaanga la Ukraine limesema limezidungua droni 78 kati ya 105 za Urusi wakati wa mashambulizi hayo.

Mamlaka katika mji mkuu wa Ukraine wa  Kyiv katika imesema kulikuwa na droni 15 zilizoilenga mji huo pekee.

Gavana wa mji wa kusini mwa Ukraine wa Odesa, OLeh Kiper amesema katika mji wake Odesa limeharibu mifumo ya umeme na kupelekea kukosekana kwa umeme kwa maelfu ya watu katika eno hilo.

Soma pia:Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana

Katikati mwa Ukraine katika mji wa Ukraine wa Poltava, droni za Urusi zimeharibu majengo ya kibiashara,  makaazi ya watu  na kuharibu pia shule ya watoto. Hayo yamesemwa na gavana wa eneo hilo Filip Pronin katika mtandao wa telegram.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW