Urusi yaishambulia tena Kiev kwa droni
30 Septemba 2024Matangazo
Mji wa Kiev na viunga vyake na eneo zima la mashariki mwa Ukraine yamewekwa katika hali ya tahadhari ya kushambuliwa kutokea angani.
Haya yanajiri siku moja baada ya Ukraine kuishambulia Urusi kwa droni zaidi ya 100 ambapo ghala kubwa la silaha lilishambuliwa, pamoja na maeneo ya ndani zaidi nchini Urusi.
Soma zaidi: Urusi yaushambulia mji wa Kiev kwa droni
Siku ya Jumatatu (Septemba 30), Rais Vladimir Putin wa Urusi alisema kwamba nchi yake itatimiza malengo yake yote ya vita dhidi ya Ukraine, huku vita hivyo vikiwa vinaingia katika mwaka wa tatu.
Wakati huo huo, Denmark imetangaza msaada wa dola milioni 194 wa kuisadia Ukraine inapokabiliana na uvamizi wa Urusi.