1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yaishambulia tena miji ya Ukraine kwa makombora

24 Januari 2024

Takriban watu saba wameuawa na majengo kadhaa ya ghorofa yameharibiwa baada ya makombora ya Urusi kushambulia miji mitatu ya Ukraine, ikiwemo miji yake miwili mikubwa - Kharkiv na Kiev.

Timu ya uokoaji katika jengo lililoharibiwa na shambulio la makombora ya Urusi, Kharkiv
Timu ya uokoaji katika jengo lililoharibiwa na shambulio la makombora ya Urusi, KharkivPicha: Ukrainian Emergency Service/AP Photo/picture alliance

Mashambulizi hayo yametokea baada ya Urusi kuukata mpango wa amani uliopendekezwa na Ukraine na washirika wake wa Magharibi unaonuia kuvimaliza vita vya karibu miaka miwili.

Maafisa wamesema kuwa, mashambulizi hayo yamejumuisha mabomu ya kuongozwa na yenye ufanisi mkubwa wa kulenga shabaha katika kile Umoja wa Mataifa ulichoeleza kuwa mashambulizi makubwa zaidi tangu mapema mwezi Januari.

Jeshi la anga la Ukraine limesema mfumo wake wa ulinzi ulifanikiwa kuzuia makombora 21.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 10,000 wamepoteza maisha na karibu watu 20,000 wamejeruhiwa tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mnamo Februari 2022.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW