1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yaishambulia Ukraine kwa ndege za droni 38

13 Agosti 2024

Jeshi la Ukraine linasema Urusi imeishambulia Ukraine kwa ndege 38´zisizokuwa na rubani na makombora mawili ya masafa marefu aina ya Iskander-M usiku kucha.

Mkoa wa Kursk
Magari ya kivita ya Urusi katika mkoa wa KurskPicha: Anatoliy Zhdanov/dpa/Kommersant Publishing House/AP/picture alliance

Jeshi la Ukraine linasema Urusi imeishambulia Ukraine kwa ndege 38´zisizokuwa na rubani na makombora mawili ya masafa marefu aina ya Iskander-M usiku kucha. Katika ujumbe ulioandikwa kwenye mtandao wa Telegram, jeshi hilo limesema 30 kati ya droni hizo zilidunguliwa katika maeneo manane ya Ukraine. Putin asema Ukraine itapokea jibu stahiki kuhusu uvamizi wake Kursk

Hata hivyo, jeshi hilo halikuweka wazi kilichofanyika kuhusiana na droni hizo nane zilizosalia. Mamlaka za eneo la Sumy zimesema mashambulizi hayo yamemjeruhi mtu mmoja na kuharibu mfumo wa usambazaji wa umeme na bomba la gesi. Baadhi ya wakaazi wa Sumy wamesalia bila umeme na gesi.

Mamlaka hizo zinasema pia kwamba jengo la hospitali na magari kadhaa yameharibiwa kutokana na mashambulizi hayo ya Urusi. Urusi imeongeza mashambulizi yake katika eneo la kaskazini tangu Ukraine ilipoanza uvamizi wake katika eneo la Kursklinalopakana na Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW