1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yaishambulia Ukraine kwa makombora na droni

Hawa Bihoga
25 Agosti 2024

Ukraine imesema Urusi imevurumisha makombora na droni kwa usiku kucha ikilenga maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Ukraine.

Makombora yalioharibiwa na mifumo ya anga ya Ukraine.
Makombora yalioharibiwa na mifumo ya anga ya Ukraine.Picha: Roman Goncharenko/DW

Aidha jeshi la anga Ukraine limeongeza kwamba droni nane kati ya tisa zilizorushwa na Urusi ziliharibiwa na mifumo ya anga ya Ukraine katika eneo la Mykolaiv. 

Kufuatia mashambulizi hayo Gavana wa mkoa wa Kharkiv mashariki Oleh Sinehubov kupitia mtandao wa telegram alisema watu saba walijeruhiwa, akiwemo mtoto wa miaka minne, huku mamlaka ya mji wa Kharkiv ikisema bomba la gesi liliharibiwa pamoja na makaazi ya raia.

Soma pia:Urusi na Ukraine wabadilishana wafungwa wa vita

Pande zote za mzozo zinakanusha kuwalenga raia na miundombinu katika vita hivyo ambavyo vilianza kwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine Februari 2022.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW