1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Urusi yaitaka Magharibi kuindolea vikwazo Afghanistan

4 Oktoba 2024

Urusi imeyatolea mwito mataifa ya Magharibi kuondoa vikwazo ilivyoweka dhidi ya utawala wa Taliban nchini Afghanistan pamoja na kuwajibika katika juhudi za kulijenga upya taifa hilo baada ya miongo miwili ya vita.

Waziri wa Mambo wa Nje, Sergei Lavrov
Waziri wa Mambo wa Nje, Sergei Lavrov.Picha: Alexander Shcherbak/Tass/IMAGO

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kidiplomasia kuhusu Afghanistan ulioandaliwa na Urusi, unaowaleta pamoja wawakilishi wa Taliban pamoja na mataifa jirani kutoka Asia na Mashariki ya Kati. 

Soma zaidi: Viongozi Asia ya Kati waitaka Ujerumani kuwatambuwa Taliban

"Marekani inaendelea kuzuia kinyume cha sheria mali za Afghanistan na kutekeleza hatua kali za vikwazo dhidi ya sekta ya benki ya nchi hii. Kwa mara nyingine, tunazirai nchini za magharibi kutambua zinalo jukumu la kuijenga upya Afghanistan baada ya mzozo, kuondoa vikwazo na kurejesha mali kwa utawala mjini Kabul." Allisema Lavrov kwenye mkutano huo.

Hata hivyo, kwenye hotuba yake, waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Urusi hakuweka bayana iwapo Urusi italiondoa kundi la Taliban kutoka orodha yake ya mashirika ya kigaidi, licha ya miito kutoka kwa maafisa wengine wa nchi hiyo. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW