1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaitaka Ukraine kuikabidhi washukiwa wa ugaidi

1 Aprili 2024

Urusi imeitaka Ukraine kuikabidhi watu kadhaa kutoka nchini humo, akiwemo mkuu wake wa idara ya usalama Vasyl Maliuk kwa madai kuwa walihusika na vitendo vya kigaidi katika ardhi ya Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin akilihutubia taifa mnamo Machi 23,2024
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Kremlin.ru/REUTERS

Katika taarifa iliyotoa jana Jumapili, wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilirudia madai kwamba Ukraine ilihusika katika shambulizi lililofanywa Machi 22 dhidi ya ukumbi mmoja wa tamasha nje yaMoscow na pia kuishtumu kwa mashambulizi kadhaa na mauaji yaliofanyika ndani ya nchi hiyo.

Urusi yaitaka Ukraine kuchukuwa hatua kwa kuzingatia mikataba

Ikitaja mikataba miwili ya kimataifa ya kupambana na ugaidi, wizara ya mambo ya ndani ya Urusi imeitaka Ukraine kutimiza ombi la hilo.

Taarifa hiyo imesema kuwa Maliuk alikiri kupanga ulipuaji wa daraja la Crimea mnamo Oktoba 2022 na kufichua habari za idara yake kuhusu mashambulizimengine ya kigaidi.

Hata hivyo, Shirika la ujasusi la Ukraine, SBU, limesema taarifa hizo kuhusu ugaidi kutoka kwa taifa ililoliita la kigaidi, hazina msingi wowote.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW