1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaituhumu Marekani kwa kuchochea mvutano

8 Januari 2026

Urusi imeishtumu Marekani kwa kuchochea mvutano na kuhatarisha usafiri wa kimataifa baharini baada ya kukamata meli ya mafuta iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Urusi katika Bahari ya Atlantiki Kaskazini.

Marekani imesema wafanyakazi wa meli ya Urusi waliokama wanaweza kufikishwa mahakamani. Picha: Handout/AFP

Marekani inadai meli hiyo ilikuwa ikisafirisha mafuta kwenda nchi kama Venezuela, Urusina Iran kinyume na vikwazo vya Magharibi. Urusi imekanusha madai hayo, ikisema meli yake ilikuwa ikisafiri kwa mujibu wa sheria za kimataifa na ilikuwa ikielekea katika bandari ya Urusi.

Wizara ya mambo ya nje ya Moscow imesema hatua hiyo "itasababisha mvutano zaidi wa kijeshi na kisiasa”, na kwamba ina wasiwasi na "utayari wa Washington kuibua migogoro ya kimataifa.”

Marekani imesema wafanyakazi wa meli hiyo wanaweza kufikishwa mahakamani, kauli ambayo wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema "haikubaliki kabisa.”

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW