Urusi yakasirishwa na Ufaransa kuunga mkono korti ya uhalifu
2 Desemba 2022Wizara ya mambo ya nje ya Urusi, imesema leo kuwa imekasirishwa na taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa iliyounga mkono mipango ya kuunda mahakama ya kushughulikia uwezekano wa uhalifu uliofanywa na Urusi nchini Ukraine.
Katika taarifa, wizara hiyo ilikosoa mipango, ambayo ingewezesha Umoja wa Ulaya kuunda mahakama maalum kuchunguza na kushtaki uwezekano wa uhalifu wa kivita wa Urusi .
Wizara hiyo imeendelea kusema kuwa inawataka wanadiplomasia wa Ufaransa ambao wako makini sana katika masuala ya haki za binadamu, kutowagawanya watu katika misingi ya ni nani yuko sawa ama sio sawa.
Ukraine imekuwa ikishinikiza kuundwa kwa mahakama maalum ya kuwafungulia mashitaka viongozi wa kijeshi na kisiasa wa Urusi inayowalaumu kwa kuanzisha vita nchini humo.