1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yalaani Putin kufananishwa na Hamas

20 Oktoba 2023

Ikulu ya Urusi, Kremlin, imesema kauli ya Rais Joe Biden wa Marekani ya kumlinganisha Rais Vladimir Putin na kundi la Hamas haikubaliki.

Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Rais Vladimir Putin wa Urusi.Picha: Pavel Bednyakov/AP/picture alliance

Biden alisema siku ya Alkhamis (Oktoba 19) Hamas na Putin wanalingana na wote wanalenga kuangamiza mataifa ya jirani zao wenye demokrasia.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, alisema siku ya Ijumaa (Oktoba 20) kauli kama hizo hazifai hasa kwa wakuu wa nchi wanaowajibika.

Soma zaidi: Biden: Kufanikiwa kwa Ukraine na Israel katika vita vyao ni muhimu kwa usalama wa Marekani

Msemaji huyo alionya kwamba tishio kwa raia wa Urusi litaongezeka mara tu Israel itakapoanzisha operesheni yake ya ardhini kwa lengo la kulitokomeza kundi la Hamas linalotawala Ukanda wa Gaza.

Peskov hakubainisha ni nani atakayeiwakilisha Urusi katika mkutano wa kilele wa amani mjini Cairo utakaojaribu kuutafutia suluhu mzozo wa huko Gaza.

Soma zaidi: Biden aifananisha Hamas na Putin katika hotuba yake

Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi (Oktoba 21).

Israel imejibu vikali mashambulizi ya Hamas yaliyowauwa wa Israel 1,400 na hadi sasa mashambulizi hayo ya Isarel yameshauwa karibu 4,000 kwa upande wa Palestina.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW