Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kwamba taifa lake halihusiki kwa namna yoyote na taarifa za kifo cha mkuu wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, katika ajali ya ndege na badala yake amenyoosha kidole cha lawama kwa Urusi. Hata hivyo, Ikulu ya Kremlin na wizara wa ulinzi ya Urusi zimeendelea kuwa kimya.