1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yaitaka AIEA kuwa na uwazi kuhusu usalama wa nyuklia

28 Agosti 2024

Urusi imelitaka Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, AIEA kuwa na msimamo wa wazi zaidi kuhusiana na usalama wa nyuklia, siku moja baada ya mkuu wa shirika hilo kutembelea kinu cha nyuklia cha Urusi.

Mkuu wa shirika la IAEA, Rafael Grossi
Mkuu wa shirika la IAEA, Rafael Grossi Picha: Roland Schlager/APA/dpa/picture alliance

Mkuu wa IAEA, Rafael Grossi ametembelea kinu cha nyuklia cha Kurskjana Jumanne na kuonya juu ya kitisho cha ajali inayoweza kutokea kwenye kinu hicho. Amesema, amekagua athari zilizosababishwa na shambulizi droni, ambalo Urusi inadai lilifanywa na Ukraine.

Shirika la habari la Urusi RIA limemnukuu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova akisema kwenye mahojiano na kituo cha redio kwamba Moscow ililitaka shirika hilo la IAEA kuzungumzia kwa uwazi zaidi suala la usalama wa nyuklia, ingawa alisema hawalishinikizi shirika hilo kuchukua mkondo wa Urusi.

Ukraine hata hivyo haijazungumzia madai ya Urusi kwamba ilikishambulia kinu hicho kilichoko katika jimbo la Kursk, karibu na mahali ambapo vikosi vya Ukraine vilianzisha mashambulizi ya kushtukiza Agosti 6 ambayo Urusi bado inajaribu kuyadhibiti.

Mashambulizi ya Urusi yameua zaidi ya watu 30 Ukraine

02:10

This browser does not support the video element.

Grossi, alipotakiwa kulaani uharibifu huo unaochukuliwa kama "uchokozi wa Nyuklia" uliofanywa na Ukraine alipozungumza na waandishi wa habari, alisema tu kwamba hakuna sababu ya msingi ya kunyoosheana vidole.

Soma zaidi: Grossi aonya kuhusu hatari ya mapigano karibu na kinu cha Kursk

Nchini Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky amesema kwa mara ya kwanza wamejaribisha kombora linalotengenezwa nchini humo, wakati wakilenga kubadilisha mkondo wa vita hivyo dhidi ya Urusi kwa kutumia silaha bora zaidi.

Zelensky alitoa tangazo hilo kwenye kongamano mjini Kyiv jana Jumanne, ingawa watengenezaji wa kombora hilo hawakutoa maelezo ya kina juu ya kombora hilo.Urusi yaishambulia Ukraine kwa makombora na droni

Waziri wa Ulinzi Rustem Umerov alisema siku ya Jumatatu baada ya mashambulizi makubwa ya Urusi nchini humo kwamba Ukraine imetengeneza silaha za masafa marefu.

Tukisalia nchini humo mkewe Zelensky, Olena Zelenska amewataka watoto wa taifa hilo kutojichukulia kama kizazi kinachovumilia magumu ya vita na badala yake wajione kama "kizazi cha washindi." 

Mkuu wa IAEA Rafael Grossi wa pili kulia akipeana mkono na mkurugenzi wa kinu cha nyuklia cha Kursk Oleg ShperlePicha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Amesema hayo baada ya ziara ya siku nzima katika kambi ya watoto wa Ukraine kwenye mji salama wa Uzhhorod na kuongeza kuwa ni muhimu kushughulikia mara moja suala la kuwasaidia watoto hao kukabiliana na kiwewe kilichotokana na vita mara baada ya kurejea kwenye miji iliyokabiliwa na mapigano.Zelensky: Ndege za kivita za Urusi ni lazima ziharibiwe

"Mke wa Rais: "Kwa kweli huu mgogoro unahitaji majibu. Na tunapaswa kuufikiria katika ngazi zote. Ninaweza kujibu kile ninachofanya kama mke wa rais. Bado ninajaribu kuendeleza ujuzi kuhusu afya ya akili nchini Ukraine. Na Ninafurahi kuona kwamba suala hili, angalau kifungu hiki, kimekuwa maarufu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka miwili iliyopita, hasa wale ambao sasa wamekuwa wahamiaji wa kulazimishwa."

Mashambulizi ya droni yamezidi kuhanikiza, wakati hii leo kukiripotiwa droni za Ukraine kushambulia matenki kadhaa ya mafuta katika ghala ya mafuta ya Glubokinskaya iliyoko jimbo la Rostov nchini Urusi.Urusi yashambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine

Hayo yanaendelea wakati Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami, NATO Jens Stoltenberg akiitisha mkutano wa Baraza la NATO-Ukraine, kwa ombi la Kyiv, hii ikiwa ni kulingana na msemaji wa NATO Farah Dakhlallah na kuongeza kuwa utawahusisha mabalozi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW